Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday 3 April 2011

Mungu Wabariki kina Mama wote !!!!!!!!!!!!!!!




Leo ni siku ya MAMA  Uingereza.Nichukue fulsa hii ya kuwatakia Kheri,Baraka,Mafanikio,Heshima,Upendo,Fadhili.
Mama yangu Mpendwa na Wamama Wote pamoja na mimi mwenyewe.Sijutii kuwa mama na Asante sana Mumewangu Isaac na Wanaume/kina baba Wote. Pasipo    ninyi  tusingeitwa mama.Pia Poleni sana mliopoteza/Kufiwa na mama,Mungu awalaze mahali pema peponi.
Mpendwa kwa kazi hizo na nyingine nyingi kila siku za kina MAMA,Tusiposaidiana na kina BABA,kweli tutapata wakati wa kupumzika?karibuni sana kwa kuelimishana na kutakiana kheri,kupongezana na unaweza kutupa kumbukumbu zako siku ambayo unahisi ulimfurahisha sana mamayako na siku uliyo muudhi sana mama yako!!.Na unapenda kumwambia nini mama yako?.MAMA NI KIUNGO CHA FAMILIA!!!!!!!!!!!

8 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kumbe ni siku ya akina mama leo hata sikujua. Ahsante Rachel basi nami napenda kuwapongeza akina mama wote duniani mojawapo wewe Rachel ,mimi na wengine wote pia mama yangu mpendwa ambaye ametutangulia kutuwekea makazi huko kwa baba yetu. Na kama alivyosema Rache tusiwasahau akina baba pia maana bila wao kweli tusingeitwa MAMA. HONGERA KWA SIKU YETU...

Simon Kitururu said...

Hongera zenu akina Mama!

Kwa MAMA yangu: Asante kwa yote!

Anonymous said...

Mama ni mtu mhim maishani,ameweza kutuzaa na kutulea tabuni,amevumilia miezi tisa tumboni,inatubidi sisi watoto tuwe karibu nao maishani,kuwasikiliza shida zao nyumbani,pindi tunapokuwa nao mbali na nyumbani,LEO HII NI SIKU YA WAMAMA DUNIANI..

Rachel Siwa said...

Asante nawe da Yasinta!
@kaka Ktururu kwa niaba ya WaMAMA wote nasema Asante!

@Mdau nikweli hakuna kama MAMA wangu!.

NAJUA WAJUA said...

Kama nilivyosema nawaheshimu na nawapenda kina mama. hongereni sana mama zetu.

Mija Shija Sayi said...

Kina mama oyeee!!

nyahbingi worrior. said...

Wabarikiwe sanasana kina mama waishio Afrika.

Rachel Siwa said...

hahahaha kaka Nyabingi vipi wasioishi Afrika umetutenga?