Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 14 February 2011

Watoto na Uhuru!!!!!!!!

Wazazi /Walezi wenzangu.Wewe una  mawazo  gani  kwa watoto chini ya miaka 15,kupewa uhuru wa kusheherekea  siku zao za kuzaliwa na rafiki zao nje ya nyumbani,tena bila ya usimamizi wetu?.Je ndiyo maendeleo,kuwapatia nafasi wajimwage au?Nasubiri mawazo yako ili tujifunze na kuelimishana katika malezi ya watoto wetu, karibuni sana!!!!!!!!!!!!!

9 comments:

SIMON KITURURU said...

Sijawahi kulea hilo nakiri! Na sijawahi kukutana na aitwaye mtoto wangu ingawa sina uhakika 100% kuwa sina kweli mtoto mahali fulani hapa duniani!


Mtazamo wangu katika hili ni:

Watoto chini ya miaka kumi na tano si vibaya kusherehekea nje ya nyumbani kama:

Muda unazingatiwa na inajulikana wako wapi na hao marafiki zao ni akina nani na huko kuna usalama gani wanakoenda kusherehekea.

Na mimi siamini kuwa kwa kuwa wako nyumbani ni sababu ya kuamini ndio salama hapo .Sana sana uwepo wao nyumbani utawapa wazazi false sense of security kujiamini hakuna kinachoendelea ingawa mengi tu huweza kutokea hapo hapo nyumbani .


Na sikuhizi na tekinolojia hizi,...
... mtoto wako unaweza kuwa unamuona hapohapo alipo nyumbani kumbe awasiliana na kibabu TAIWAN ambacho kinamzengea mbele yako bila wewe kustukia kwenye SIMU na KOMPYUTA.

Na kitekinolojia naamini watoto huwa werevu kirahisi kuliko WAZAZI kitu ambacho labda kwa kuwa unawaangalia WATOTO kwenye SHEREHE yao nyumbani na kusikia wanayoongea,..
....lakini bado waweza kukuta LUGHA waongeayo haifanani na YAKO kutokana na matumizi ya maneno na MISAMIATI kitofauti kwa hiyo HUELEWI kikweli kuwa wasemayo ndiyo WAMAANISHAYO na wafanyayo HUYAELEWI kwa kuwa kikucheza na tekinolojia wameguzidi .

Hujawahi kustukia kuwa hata LUGHA na misamiati mara nyingi hutofautiana kati ya WAZAZI na WATOTO?


Na nikijichukulia mimi mwenyewe kama mfano wa yawezayotokea hapohapo nyumbani - Ngono mara ya kwanza nilifanyia nyumbani CHAPCHAP kidakika tu chache kama ilivyo kwa wengi VIDUME wakati wanajifunza FANI wakati watu wengine wako tu hapohapo nyumbani sebuleni.


Na wakati nilivyokuwa mdogo zaidi ya hapo nilikuwa nalazimishwa kulala mchana! Na kilichokuwa kinatokea ni kuwa nilijua ni saa ngapi wazazi wanarudi .

Kwa hiyo ilikuwa na taimu tu dakika kama tatu hivi kabla WAZAZI hawajaingia nyumbani wakati nimeshawaona au kuwasikia ndio najifanya nimelala halafu wakija kuniamsha najifanya kuwa ndio naamka kumbe wala sikuwa nimelala. Na jambo hili liliendelea muda mrefu mpaka MAMA ndiye akastukia huwa si lali na nafikiri BABA mpaka leo anafikiri nilikuwa kweli nalala mchana.:-(

Na nakumbuka enzi za O-level Morosec hasa kutokana na ukweli nilikuwa nafaulu darasani na nikawa naruhusiwa kwenda kujisomea usiku hasa na RAfiki yangu mmoja aitwaye ISAYA JELLy ambaye sijui yuko wapi siku hizi! Nilikuwa nakwenda kweli kujisomea na naamini kwa kuwa nilikuwa naaminiwa kwa hilo, hakuna hata siku moja nilidai kuwa nakwenda kusoma na sikwenda kusoma kweli kisa uhuru na ilijulikana nyumbani nahusudu kusoma na kufaulu. Ndio miye ni miongoni mwa wale ambao wazazi walikuwa wananishauri nipunguze kusoma vitabu na kufanya mambo mengine kwa kuwa hasa BABA alikuwa hapendi kunikuta mitaa ya saa tisa usiku bado nasoma kitu iwe stori tu za WILLY GAMBA au kitu kingine kama KEMIA n.k


HITIMISHO:

Kama umewalea wanao vizuri na unawaamini wapangie muda kwa mfano mwisho kuwa nje saa moja na nusu , jua marafiki zao na jua wanapokwenda kusherehekea, wape UHURU pale wanapostahili!


Pia ni vizuri kukumbuka halihalisi kuwa hata ufanyeje kama mzazi, huwezi kuona kila kitu kinachoendelea kila wakati hapo nyumbani pia.


Ni mtazamo tu!

Swahili na Waswahili said...

Mmmmhhhhh @kaka yangu Kitururu!! nashukuru sana kwa mawazo yako,ninahakika yatanisaidia mimi na wengine pia, yaani umefafanua na ukweli saanyingine unauma,kunasehemu umegusa yaani mpaka mzazi/mlezi anafungua macho zaidi!

kama ya kibabu cha TAIWAN!Mhhh kaka sina la kusema.

KAKA NATAMANI KUSHEHEREKEA HARUSI YAKO,PIA KUPATA KINA SHANGAZI MAPEMA,NINI TATIZO?

SIMON KITURURU said...

Tatizo sijatulia!:-(

Yasinta Ngonyani said...

Naona Kaka Simon kamaliza kabisa hata kama anasema hana mtoto na hajawahi kule lakini hapo umetoa bonge la darasa. Binafi nisingependa watoto chini ya miaka kumi na tano wawe na shrehe bila uangalia. Yaani unaweza kuwa pale ila si muda wote ili kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa. kwani ni moja ya wao kujifunza maisha.

Mija Shija Sayi said...

Kitururu sidhani kama tatizo ni kutokutulia, mimi nadhani unachagua sana...kweli si kweli?

Ila wazazi kazi tunayo, na tena siku hizi balaa zaidi kwa watoto wa kiume maana hawa kina TAIWAN hawachagui wala kubagua..

Tuombeane wajameni.

Mija Shija Sayi said...

Haya da Rachel soma hii link tuhitimishe anayoyasema Mtakatifu Kitururu, mwanao anapitiwa hapo hapo nyumbani.

http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/fumanizi-3

Swahili na Waswahili said...

Mwenzangu kazi ipo!nimeingia wangu dent anafatwa mpaka home,kazi ipo da Mija!

Hayo maoni ya kaka Kitururu yamewagusa wazazi wengi jana kuna rafiki yangu amesoma, akashindwa kuvumilia akaona anipigie simu,
anasema huyu kaka amenigusa haswa!

emu-three said...

Birthday, au siku ya kuzaliwa...niliwahi kumuuliza babu yangu yangu kuwa aliwahi kusherehekea siku yake ya kuzaliwa. Alisema, `ili iweje..'
Watoto ni watoto, kama mzazi tuna dhamana kubwa sana, kwani sasa hivi kwasababu ya `utandawazi' watoto wanakuwa `werevu' kupita umri wao, baya zaidi wanaiga `yale yanayowaharibu' baadaye!
Babu yangu alisema `ili iweje..' hakutaka kuendelea kuelezea zaidi, na sasa natafakari kuwa `hizi sherehe zenye `gharama kubwa' ikiwemo birthday, nini inamfundisha mtoto? sio kwamba napinga, ila natafakari kiundani.
Natafakari kwasababu , utoto una-udadisi sana, hasa wa mambo mabaya, kuanzia nyumbani hadi huko atakapokwenda, ...ukimruhusu aende atakutana na `walimu dunia' naye siku baadaye utakuta kabadilika, ukimkataza, `atakutana na mwalimu runinga, ...hapo habanduki...sasa tufanyeje?
Jibu ni kuwa wewe ni mzazi na huyo ni mtoto...samaki mkunje akiwa mbichi!

Swahili na Waswahili said...

Hapo sasa kipi chema kwetu,pia babu akikwambia hivyo ujue hataki hayo mambo!@ emu-three.

Ahsante sana,Tuendelee!