Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday 9 February 2011

Wanawake na Mitindo!!!!!!!!!!!!!!!!



Haya wapendwa!Mitindo hii wewe unaionaje au ndiyo kwenda na wakati?.
Je mitindo inatakiwa iendane na sehemu usika? Yaani kama kwenye, Harusi,sokoni,bar na kwingineko.
Wewe unamawazo gani na Mitindo ya kina mama//dada? Tuhabarishane  wapendwa!!!!!!!!

8 comments:

Mija Shija Sayi said...

Aiseee!! huyo dada mwenye rasta kanifanya nifikirie kuzirudisha za kwangu.

Kuhusu swali lako kwa kweli wengine wanapatia kuvaa kulingana na wakati wengine wanafanya makusudi tuu kutafuta attention..

mumyhery said...

mimi nilikuwa nafikiria hivyo kila nguo unavpovaa inategemea na sehemu uendayo , lakini siku hizi kuavaa nguo inategemea na mtu pendavyo!!!

Anonymous said...

Nguo kama hio si bora atembee uchi tu huu ni ukosefu wa adabu.

emu-three said...

Mmmmh, wanawake live...semeni wenyewe tusikie!

Simon Kitururu said...

Mitindo kwa watu wengine ni KAULI kwa hiyo uvaaji kuna kitu unaongea!

Kwa ujumla naamini lakini kama unaijua JAMII na TAMADUNI zake na hutumii mitindo KUONGEA kwa makusudi KITU inasaidia kama mitindo itaenda na sehemu husika kama UNAZIJUA hizo sehemu husika. Hii inaweza kukusaidia kutochanganya watu na kutunza heshima yako!


Ila wanawake kwa ujumla ni wazuri sana nyie na wala haihitaji hata mitindo ya ajabuajabu ili UZURI uumuke vizuri!

EDNA said...

Mitindo ni lazima iendane na wakati na mahali kwa mfano huwezi vaa kama huyo dada hapo mwisho ukaenda kanisani/msikitini au sehemu yoyote ya ibada.Hizo rasta hazina tatizo mahali popote unatinga zazo.

Anonymous said...

Mie hizo rasta nimezipenda!

Mama Malaika

Rachel Siwa said...

Ahsanteni wapendwa kwa maoni yenu!
mama Malaika karibu sana ndugu yangu!