Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday 19 January 2011

Unapokuwa na mawazo faraja yapatikana wapi?



Yaweza patikana kwa kusoma  vitabu,  kwenye mikusanyiko,kuwapekeyako au?
Nasubiri kwako msomaji maana kila mtu ana mawazo ila kuna yanayochanganya!!!!!!!!

21 comments:

Simon Kitururu said...

Mie nikikereka KITABU hakipandi na kuwa peke yangu au na watu wenye huzuni huwa sipendelei kwa kuwa huwa wanamchezo wakuniongezea mawazo hasi,....
....na ni kujichanganya na watu wenye furaha hasa wachekeshao ndio hupendelea.

EDNA said...

Mimi nikiwa nahudhuni,ninachofanya nikusikuliza muziki ule ninaoupenda au kuongea na mtu /watu ambao naweza kuwashirikisha kupunguza mzigo wa hudhuni.

Mzee wa Changamoto said...

Da Rachel... Muda sijajikita hapa lakini sasa nimebarikiwa pata muda "kurejea nyumbani".
Mimi niwapo na majonzi mimi ni REGGAE tu.
Yaani hapo ndipo ninapojipata kila ninapojipoteza.
Wewe je?

Yasinta Ngonyani said...

Mimi nikiwa na mawazo/huzuni navaa mavazi yangu ya kufanya mazoesi na kuanza kukimbia huku nikisikiliza mziki niupendao. Nawe je Da´Rachel?

Rachel Siwa said...

hahahaa@kaka Mubelwa na da Yasinta nimeipenda hiyo na weweje?

Mimi nikiwa na mawazo napenda kusikiliza miziki au kutoka yani kuwa nje ya nyumbani,hiyo ndiyo faraja yangu.

pia nitajaribu kila faraja ya mtu hapa nione tofauti.

@kaka Kitururu hata mie kitabu hakipandi naona bluuu tuu!

@dada Edna hiyo powa wangu!

@kaka Mubelwa nimefurahi kkukuona tena hapa kwako najua umetingwa na masomo nilikusoma!!.

Nawewe msomaji uliye baki je?

JOSHUA PHILEMON said...

MUNGU NDIYO MFARIJI WA KWELI . MAMBO MENGINE YANASAULISHA MWILI KWA MUDA MFUPI, LAKINI HAYALETI FARAJA AMBAYO ITAONDOA MAWAZO YALIYO MOYONI.LAKINI MUNGU HULETA MAJIBU YA SHIDA UNAYOWAZA· HALI YA KUMTAFUTA MUNNGU IMEPUNGUA NDIO TUNAUNDA MAMBO YETU ILI KUONDOA MAWAZO

Rachel Siwa said...

Aksante sana kaka Joshua kwa ushauri wako mzuri!karibu sana.

emu-three said...

Wanasema kuwa rafiki wa kweli ni maneno ya mungu, basi mimi nikizidiwa na mawazo, nasoma maneno ya mungu, nikitaka kuongea kuondoa hayo mawazo naswali,(naongea na mungu)
Kama ni mawazo ya kawaida, mmmh, nayatungia kisa, nikizama kwenye kuandika, basi weee, mawazo yote huhamia kwenye karatasi au mtandaoni,(kwenye computa)

Simon Kitururu said...

Naonea wivu sana ambao kwao MUNGU au maneno ya MUNGU ni kimbilio la kila kitu. Mie mara nyingi kwa kufikiria MUNGU ndio huzinguka.

Kwangu hakuna kitu kigumu kuelewa na kufarijika nacho kama MUNGU hata kupitia kile tuhubiriwacho kuwa ni mapenzi tu ya MUNGU kwanini chamoto mtu unakiona!:-(


Tuombeane!

Mija Shija Sayi said...

Dah! Kitururu hapa mwishoni umenitia mawazo hata faraja sijui pa kuipata sasa...

Labda swali moja kwako, tuombeane kwa nani?

Simon Kitururu said...

@Da MIJA: Samahani kwa kuingilia vipengele vya msuuzo wa roho yako!:-(

Hapa naongelea tuombeane kwa MUNGU ,...
....kwa kuwa ndiye nisikiaye ni MUWEZA yote ingawa kuna washuhudiao kuwa shetani naye labda ni bonge la mjanja ukifikiria ni jinsi gani inasemekana anapatia ya WANADAMU kwa mtazamo wa KIBINADAMU!:-(


LAKINI tukiachana na MKAO wa mtazamo huo,...

...kwa bahati mbaya yasemekana katika KUOMBA inawezekana kama nia ni CHUMVI ni rahisi kupata chumvi kwa mwenye CHUMVI,...


.... kwa hiyo labda kama DAWA katika nia ya MTAKA KUTULIZA MAWAZO ni kidude,....


... yasemekana kwa KUOMBA mwingine kama MUNGU ni kujaribu tu kubadili wazo ili UTAKACHO kisiwe na makali vile kwakuwa labda kwa mtuliza MAWAZO kwa kidude,...

...DAWA yenye uhakika ni kwa huyo mtu kupewa KIDUDE!:-(


Swali:
Kwani si inasemekana MUNGU huwa hatimizi kila kitu hasa kwa kuwa kuna mengi binadamu wahitajiyo kutuliza MAWAZO labda bado KWA WAFUATA ya MUNGU hayo ni DHAMBI?

Rachel Siwa said...

Aksante emu-three! nakuaminia kwa kutunga visa wewe na ukiwa na mawazo naona spid inaongezeka!

@aksanteni kaka Kitururu na da Mija nimefurahi kuona manaeleweshana kuhusu Mungu nasi wengine tunaendelea kujifunza!

Tuendelee!

Mija Shija Sayi said...

Kitururu umesema kweli kwamba kama unataka chumvi ni rahisi kupata kwa mwenye chumvi... lakini tatizo linakuja pale huyo mwenye chumvi anapokataa makusudi kukupa haja yako. Na mimi nadhani huo ndio huwa ni mwanzo wa MAWAZO anayoyaongelea dada rachel...., Mtu unashida mwenye uwezo wa kukusaidia anakubania Faraja unaipata wapi????....Huoni hapo dawa ni kumtafuta asiye mchoyo??? MUNGU!!!!

Simon Kitururu said...

@DA MIJA :


Nilikubali yote mpaka ulipofikia hitimisho kuwa MUNGUawezaye na MWENYE UWEZO WA YOTE ndiye sio MCHOYO!:-(

Si unajua sifa karibu zote zijulikanazo kwa WAKRISTO hata wasiostukia kuwa MUNGU WAMUOMBAYE ana wivu ndio maana kuna mambo MUNGU wa wakristo anachukia tu ifananavyo na WAKRISTO KIUBINADAMU WAO hata wale wasioamini ni BINADAMU ,...

...LABDA NDIYE aliyetunga aidia ya MUNGU.:-(

Sasa kama MUNGU ndiye achomaye mpaka watu waliomkosea moto,....


.... watu ambao yeye hata kama ndiye ajuaye ya DA MIJA hata kabla DA MIJA hajazaliwa ndiye ambaye DA MIJA akionjwa kwa kuwa tu katongozwa na NA MJANJA ALIYESTUKIA UDHAIFU WAKE kuwa sio MCHOYO au tu ule udhaifu wake wa kibinadamu MWINGINE wa kuwa ukikosea cha kuomba na wakati hajisikii vizuri ni MCHOYO,...

....akakubali na AKAKUBALI TU moja ya tamu za KIBINADAMU ambayo wajifanyao wanamjua MUNGU ni DHAMBI kabla hajafa....



SAMAHANI!

SI ukijiweka kwenye viatu vyangu unaweza kugundua SASA HIVI kwanini niliomba kuombewa katika COMMENT FULANI HAPO JUU,...

... na kwa hilo ukafikia uamuzi kama mimi labda MUNGU ni bonge la ambayo tukiyaingia KICHWAKICHWA ,...
.... hasa kwa kuwa nasoma vitabu vyote vya wajanja wamnukuuye na WANUKUUVYO labda,...

...huwa NI KWANINI nahisi ya MUNGU labda niwaachie tu waaminio MUNGU na kwa kuwa wanaamini katika sala labda waniombee tu kitu fulani ambacho labda KUNA UWEZEKANO kwa KUJUA NAWAZIDI ingawa labda ni imani ndio bonge kwa yoyote aliyezidi?


Swali KWA Da MIJA:
Mungu aaminikaye anauwezo wakuachia watu waende JEHANAMU kuchomwa hudhani labda anaweza kuwa ni MCHOYO?:

BADO NI wazo tu hili !:-(

Unknown said...

mmh! naona nimechelewa hii hoja... Mimi hupendelea kufanya mazoezi huku nikisikiliza muziki... ka Dada Yasinta vile...

emu-three said...

Hivi Rachel upo darasa la ngapi, maana hiyo picha...mmh, au ni ya mwanao nini? mjadala uendelee jamani, naona wataalamu wa kuhubiri waingilie kati, kuna watu wanataka kumjua mungu!

Rachel Siwa said...

@da Mija mimi kwasababu naamini katika Mungu yupo najua itakuwa tiba kwangu!

@kaka Kiruru vipi na wazazi wanaowachoma vidole au mikono watoto wao labda wameiba sukari.....je wote ni mama wakambo?maana wengine wamewazaa wenyewe je hawa nao tuwaweke fungu gani?.....

@kaka Mrope hujachelewa,Asante kwa mchango wako!!

@hahahaha emu-three umenichekesha kweli,huyo ni mwanangu au ningependa kusema mwanetu si mtoto wangu ndiyo wako?aksante sana nitajiweka ili unione tusije pishana njiani!!!!!!


aksanteni da @da Mija na kaka Kitururu kwa michango yenu nasi tunajifunza zaidi nawengine rukhsa kuchangia unaloona kwako lina manufaa linaweza kusaidia na wengine!!!!!

Tuendelee na wewe jee?

Mija Shija Sayi said...

Jibu kwa kaka Simon.

Ninaamini Mungu kama mzazi hamnyimwi mwanaye kitu kwa nia mbaya. Anapotunyima tukitakacho huwa ni kwa ajili ya manufaa yetu wenyewe kwa vile ninaamini anaona mbali zaidi yetu.

Kwa mantiki hii basi, ninakataa kabisa kuwa Mungu anaweza kuwa Mchoyo.

***My friend unajua kujieleza si mchezo au rachel unasemaje?

Rachel Siwa said...

hahahha @ da Mija Chezea yeye kaka KItururu!!

Anonymous said...

Mimi nikiwa na mawazo au kukwazwa jambo lolote huwa nasikiliza huu wimbo wa Neema mwaipopo unaosema raha jipe mwenyewe.
http://www.youtube.com/watch?v=kQDs3A3NdDQ&feature=related

Rachel Siwa said...

@mdau hapo juu nami nitausikiliza huo wimbo,Asante sana!