Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Swahili na Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 11 January 2011

Je matendo yako ya utotoni yanafanana na watoto waleo?

kuvaa nguo za kufanana,,kunywa maji kwa kikombe kimoja, kugombea kitu kama mimi nimekiwahi hiki na vingine vingi!!!!!!!!!!!

11 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Hayafanani, kwa sababu mambo yamebadilika. Huu ni ulimwengu wao - ulimwengu wa kizazi kipya, ulimwengu wa miziki ya kufokafoka, ulimwengu wa kuvaa milegezo, ulimwengu wa facebook na Google, ulimwengu mpya.

Hata hivyo kwa vijijini nadhani mambo uliyoyataja bado yapo ingawa nako pia yanabadilika kwa kasi.

Yasinta Ngonyani said...

Hakika nakubalina na kaka Matondo haya hayafanani kabisaaaa yaani huu ni uölimwengu mwingine kabisa.

Anonymous said...

Sikuhizi wanagombea mambo tofauti, remote, nataka kuangalia programme hii, zamu yangu kutumia computer nk.

emu-three said...

Mhh, hayafanani, ila `utoto' unafanana. Siku hizi mambo yamerahisshwa, kwahiyo vichwa vinataka `urahisi' lakini enzi za utoto wangu, mmmh, inabidi uwajibike kweli kwahiyo kichwa kilikuwa kichwa kweli....

Mcharia said...

HAPA NINA NUKUU:
Leo nimekumbuka nilipokuwa mdogo kwenda mstuni kuokota kuni, na hapo ujue ukirudi inabidi uende mtoni/kisimani kuchota maji. Wakati huo huo maharage yapo jikoni inabidi uchochee na kisha inabidi kutwanga mihogo. Ama kweli tumetoka mbali!!! Haya ndio maisha tuliopitia wengi huwa najiuliza sijui ni muda gani nilisoma?....!!MWISHO WA KUNUKUU.

Nukuu...niliikuta hapa: http://ruhuwiko.blogspot.com

Unaweza kuvuta hisia na kupata picha halisi ya sasa?

Mija Shija Sayi said...

Da Rachel teknolojia imebadili mambo, siku hizi wafanyabiashara wamegundua hadi kuchapisha majina kwenye vikombe, unafikiri hapo kuna cha kugombania kikombe hapo?...

Ubarikiwe.

Mfalme Mrope said...

mambo yamekuwa tofauti sana siku hizi. Kama walivyonena walionitangulia, teknolojia imefanya mambo mengi kuwa rahisi na hivyo kuwanyang'anya watoto wetu michezo mingi tuliyocheza!!

SIMON KITURURU said...

Mmmmh!

Swahili na Waswahili said...

Aksanteni sana wapendwa kwa michango yenu na ufafanuzi wenu!
@ka Kitururu mbona umeguna tuu?

sasa hapo ipi bora matendo ya sasa au yazamani.

kwangu mimi si vyote vya sasa ni vyema kwani yapo mengi sana ya zamani ni mazuri sana!!!!

mbarikiwe sana!.

Anonymous said...

Da Rachel, una watoto bomba!!!!! kama mama yao!

Swahili na Waswahili said...

hahha Asante mpendwa!!!!!!!