Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday 30 December 2010

Kukaa kiti cha mbele karibu na dereva ni heshima au starehe?

9 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kwa mimi ni mradi nifika niendako salama....

Mija Shija Sayi said...

Mmmmh hii ya leo ni falsafa ngumu Rachel, tungoje tuone Kitururu ana maoni gani.

Unknown said...

Hii ni ngumu kidogo lakini nafikiri inaweza ikaja kwa majibu matatu. Kwanza, kuna wanaodhani kuwa ni heshima. Pili kuna wanaodhani kuwa ni starehe, na tatu wengi wetu bora tufike kule tunakokwenda. Ila swali hili nadhani laweza fika mbali.

Simon Kitururu said...

Kukaa kiti cha mbele inaweza kuwa ni vyote: HESHIMA au STAREHE kutegemea tu na tamaduni, STATUS au tu pia mengine mengi.

Ukifuatilia historia ya swala utagundua :

Magari yalianza kuingia kwa matajiri enzi hizo yakichukua nafasi ya farasi zivutazo vijigari ambavyo kwa kawaida msafiri wa hivyo alikuwa na muendesha farasi wake mbele kwenye farasi na tajiri mwenyewe kuwa NDIYE YULE nyuma kwenye kijimkokoteni maalumu aka kijigari.


Na kwa hiyo magari yalipoingia, bado ikawa hivyo hivyo kuwa MHESHIMIWA anakaa nyuma na dereva mbele.Ikiashiria kukaa nyuma ni HESHIMA.


Na ukifuatilia mpaka leo utaona maeneo mengi kuanzia Uingereza mpaka CHINA kama wewe ni KIBOSILE siti yako ni nyuma.

Ila kama ijulikanavyo kuwa kuna waheshimiwa wapendao kuendesha wenyewe au tu ndio wenye magari.

Kwa hiyo ukipewa lifti na umuheshimuye ni heshima kukaa mbele na yeye kwa kuwa ukikaa nyuma kiaina kunawatafsirio unamchukulia kama dereva wako na kwa hiyo humheshimu.


Tukirudi Marekani na kusoma mpaka historia ya Rosa Parks na WAMAREKANI weusi- utastukia kuwa WEUSI waliokuwa wanadharauliwa nafasi yao ilikuwa ni NYUMA ya basi au tu Malori.

Na kama umeshawahi kusafiri na basi au Lori kwenye barabara mbovu kama miye utagundua ni kwanini nyuma wanasakiziwa walalahoi kwa kuwa pekechapekecha yake si yakitoto utarushwa mpaka kiporo cha jana kitake kutoka kama dereva hawajali- kitu kifanyacho kukaa mbele kwenye basi au LORI huonekana ni starehe na heshima kuliko nyuma ya basi.

Na KWA WATOTO mbele ya gari ndiko kwenye mambo yote.Kwanza unaona mbele halafu unaweza kumuigilizia dereva kuwa nawe unaendesha gari!Kwa hiyo kwa watoto mbele ni STAREHE ingawa toto dogo sana bado yashauriwa likalishwe kwenye kiti maalumu nyuma KIUSALAMA.

Hitimisho:
Si umeona sasa kiti cha mbele au tu mbele kuwezavyo kuwa na tafsiri zote KIHESHIMA na kistarehe?

Kwani darasani wewe ulikuwa unapenda kukaa wapi? Mbele karibu na mwalimu au nyuma ambako mtu unaweza kujidanganya mwalimu hakuoni vizuri hata kama unatumia mlungula?


Kheri ya Mwaka mpya Rachel!

Mija Shija Sayi said...

Heee!! Watu mna mawazo jamani! Kirururu umeelezea vizuri sana hata sikuyafikiria yote hayo.

Rachel tukirudi katika picha inaelekea hao watoto wanagombania kukaa mbele au?

biggytime said...

ni starehe sana tu, kwani unakaa kuona ya mbele zaid na mengine we wanyuma hutoyaona ata ukiyaona basi hahahaha..na vile vil raha raha tu kueka kisambusa ukikaa mbele..heheheh

Anonymous said...

Kukaa mbele ni hali ya ufahali(Status)nikitolea mfano kwa wasafiri kwa njia ya TUNDURU-SONGEA kuna usafiri wa Landrover 109 au 110 kipindi hicho nilichopita 2005 nilkuta usafiri huo ukiwa katika makundi matatu kiti cha mbele kwa dereva iligharimu shilingi 30000 kwa abiria, siti za kati watu 4 kila mmoja 20000 na kule nyuma kabisa ilikuwa shilingi 15000.yote hii ilitegemea na nafasi na utulivu aupatao abiria kwani mbele waweza hata kukata/kutoa KISHIKA kama vile gari ni mali yako.

Rachel Siwa said...

Aksante wapendwa wote kwa ufafanuzi wenu!@ da mija ulisema unangoja kaka Kitururu,Ulijuaje kama anajua kufafanua hii mada kiasi hicho?
kuhusu hao watoto mwenzangu huo ni ugomvi wa kukaa mabele hauishi!

Kheri ya mwaka mpya na nawapenda wote!

Anonymous said...

Nikufika upesi uendapo.